Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mikataba hiyo ni sehemu ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi mbili kwa lengo la kukamilisha miradi 184 ya ujenzi nchini Libya iliyokwama ikutokana na vita vya ndani.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kusaini mikataba hiyo, Waziri wa Mipango wa Libya Tahir Jahaimi amesema kuwa, Uturuki ina nafasi kubwa katika utekelezaji wa miradi ya kiuchumi ya Libya.
Kwa upande wake Waziri wa Biashara wa Uturuki Ruhsar Pekcan amesema kuwa, mikataba hiyo ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi yake na Libya itaandaa uwanja mzuri wa kupatiwa ufumbuzi masuala mbalimbali na kuwezesha uwekezaji katika miradi mipya nchini Libya.
Naye Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Akiba wa Libya amesema kuwa, anataraji kuuomba Umoja wa Mataifa uruhusu mfuko huo kutoa mabilioni ya dola za Libya yaliyoko katika akaunti mbalimbali yaliyozuiliwa baada ya Libya kuwekewa vikwazo.
Libya ambayo ilitumbukia katika vita vya ndani baada ya kuondolewa madarakani utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, ina serikali na mabunge mawili. Bunge moja lina makao yake katika mji wa Tobruk mashariki mwa nchi, na bunge jingine liko Tripoli.
342/